- Version
- Download 340
- File Size 616.06 KB
- File Count 1
- Create Date August 11, 2022
- Last Updated August 11, 2022
Taarifa Fupi Kuhusu Mfuko wa Dhamana wa Jamii Ya North Mara (NMCTF)
Kuhusu Mfuko
Mfuko wa Dhamana ulisajiliwa tarehe 28/05/2012 nchini Tanzania chini ya sheria ya nchi namba 318 ihusuyo usajili wa udhamini na kupatiwa hati ya usajili namba 4445.
Mfuko ulianza shughuli zake rasmi tarehe 02 April, 2013 Kwa kuajiri watendaji mbalimbali wakiwamo Meneja wa Mfuko kwa ajili ya Kusimamia ofisi na shughuli mbalimbali za Mfuko.
Muundo Wa Mfuko
Mfuko wa Dhamana wa Jamii ya North Mara (North Mara Community Trust Fund), uliundwa na Makampuni ya Keng’anya Enterprises Limited and North Mara Gold Mine Ltd.
Makampuni haya kwa mujibu ya sheria ya mifuko ya dhamana, yalitengeneza Hati ya Kuhamisha Mali kwenda kwa Wadhamini (TRUST DEED), ambapo ilisajiliwa na Wadhamini sita (6) kateuliwa kwa ajili ya hii dhamana. Wadhamini (Trustees) 4, wanawakilisha wachangiaji (wadhamini KEL – 2, NMGM – 2) na Wafadhiliwa (beneficiaries), wadhamini 2.
Mamlaka na Maamuzi yote ya shughuli za uendeshaji wa Mfuko yako chini ya Bodi ya Wadhamini wa Mfuko (Board of Trustees). Bodi inaongozwa na Mwenyekiti ambaye hutokana na moja ya wachangiaji wa Mfuko (KEL na NMGM), kila mwaka kwa kubadilishana.