North Mara Community Trust Fund – North Mara development for the country
North Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust Fund
Maendeleo ya Mara Kaskazini ni Maendeleo ya Tanzania
North Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust Fund
North Mara Community Trust Fund (NMCTF)

Mfuko wa Dhamana wa Jamii ya North Mara

Mfuko wa dhamana wa North Mara ni matokeo ya mgongano wa kimaslahi baina ya Keng’anya Enterprises Limited (KEL) yenye hati usajili namba 17118 na Placer Dome (T) Limited (PDT) yenye hati ya usajili namba 23446 (awali ilijulikana kama Afrika Mashariki Gold Mines Limited na sasa ni African Barrick Gold). Mgongano huu unarejea shauri nambari 298 ya mwaka 1997 na 315 ya mwaka 2002 yaliyoamuliwa nje ya mahakama na kusajiliwa mahakama kuu ya Tanzania, mnamo mwezi Desemba 2004.

KEL na PDT pamoja na mambo mengine, walikubaliana kuanzisha Mfuko wa Dhamana uliotarajiwa kuanza Januari 2006 kwa ajili ya kusaidia vijiji vitano vya Kerende, Nyangoto, Nyamwaga, Genkuru na Kewanja vilivyo na mkataba na mgodi wa North Mara.

Ufadhili wa vikundi vya Kuondokana na umaskini
Kuanzisha Maabara za Kompyuta
Teknolojia Ya Habari Na Maelezo (TEHAMA)
Mabweni Ya Wasichana
Uwekezaji katika Kilimo cha Miwa

Michango

Shiriki kuchangia shughuli za kimaendeleo na kijamii za Mfuko wa Dhamana wa Jamii ya North Mara (NMCTF)

Wachangiaji na Wanufaika wa NMCTF

Wachangiaji pekee katika huu mfuko (wafadhili) hadi sasa ni wawili tu;  NORTH MARA GOLD MINES (NMGM) pamoja na KENG’ANYA ENTERPRISES (KEL). Vijiji havijawahi kuchangia huu mfuko na wala hakuna kiasi chochote cha fedha zitokanazo na mrahaba wa vijiji zilizowahi kuingizwa na mgodi katika mfuko huu.

Wanufaikaji wa mfuko huu ni vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa North Mara, ambavyo ni; Nyangoto, Kewanja, Genkuru, Nyamwa-ga na Kerende.

DIRA

Kuwa Mfuko Wa Dhamana ulio bora nchini Tanzania ambao kwa ufanisi unahamasisha, unasaidia na kuunga mkono miradi na shughulu za jamii katika Nyanja za elimu, afya, kilimo, maji na kupambana na umasikini.

DHAMIRA

Kutafuta raslimali za kutosha kwa ajili ya kusaidia miradi na shughuli za jamii zinazolenga kuinua, kuendeleza na kuunga mkono hali ya maisha ya uchumi endelevu katika jamii ya North Mara kwa muda mrefu mbeleni hata baada kumalizika na kufungwa kwa shughuli za mgodi.
North Mara Community Trust Fund (NMCTF)

Neno Kutoka kwa Mkurugenzi

Wazo kuu lililopelekea kuundwa Mfuko lilitokana na ukweli kwamba, baada ya Maisha ya Mgodi kwisha, kuwe na chombo mbadala kitakacholeta chachu ya maendeleo na uwepo wa maisha kiuchumi (livelihood). Hivyo basi Mfuko ukaanzishwa ili uwe chombo endelevu kitakachosaidia kutoa huduma mbalimbali za kijamii, na kuchangia maendeleo ya jamii, hasa pale Maisha ya Mgodi yatakapokuwa yamefikia ukomo.

Mfuko wa Dhamana una jukumu la kuhamasisha, kusaidia na kutoa msukumo kwenye miradi na shughuli katika nyanja za elimu, mafunzo, afya, kujenga uwezo, kilimo, maji na kuondoa umaskini kwa kadri wadhamini watakavyoona inafaa.

KARIBUNI
NORTH MARA COMMUNITY TRUST FUND

– Kwa Maendeleo endelevu ya Jamii ya North Mara

Mr. John S. Mhagama
Meneja wa Mfuko

Machapisho Mapya

NMCTF Brochure

616.06 KB 301 Downloads