Kuhusu NMCTF – North Mara Community Trust Fund
North Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust Fund
Maendeleo ya Mara Kaskazini ni Maendeleo ya Tanzania
North Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust FundNorth Mara Community Trust Fund

About us

North Mara Community Trust Fund (NMCTF)

Mfuko wa Dhamana wa Jamii ya North Mara

Mfuko wa dhamana wa North Mara ni matokeo ya mgongano wa kimaslahi baina ya Keng’anya Enterprises Limited (KEL) yenye hati usajili namba 17118 na Placer Dome (T) Limited (PDT) yenye hati ya usajili namba 23446 (awali ilijulikana kama Afrika Mashariki Gold Mines Limited na sasa ni African Barrick Gold). Mgongano huu unarejea shauri nambari 298 ya mwaka 1997 na 315 ya mwaka 2002 yaliyoamuliwa nje ya mahakama na kusajiliwa mahakama kuu ya Tanzania, mnamo mwezi Desemba 2004.

KEL na PDT pamoja na mambo mengine, walikubaliana kuanzisha Mfuko wa Dhamana uliotarajiwa kuanza Januari 2006 kwa ajili ya kusaidia vijiji vitano vya Kerende, Nyangoto, Nyamwaga, Genkuru na Kewanja vilivyo na mkataba na mgodi wa North Mara.

Ufadhili wa vikundi vya Kuondokana na umaskini
Kuanzisha Maabara za Kompyuta
Teknolojia Ya Habari Na Maelezo (TEHAMA)
Mabweni Ya Wasichana
Uwekezaji katika Kilimo cha Miwa
Tufahamu zaidi
Wachangiaji na Wanufaika wa NMCTF

Wachangiaji pekee katika huu mfuko (wafadhili) hadi sasa ni wawili tu;  NORTH MARA GOLD MINES (NMGM) pamoja na KENG’ANYA ENTERPRISES (KEL). Vijiji havijawahi kuchangia huu mfuko na wala hakuna kiasi chochote cha fedha zitokanazo na mrahaba wa vijiji zilizowahi kuingizwa na mgodi katika mfuko huu.

Wanufaikaji wa mfuko huu ni vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa North Mara, ambavyo ni; Nyangoto, Kewanja, Genkuru, Nyamwa-ga na Kerende.

DIRA

Kuwa Mfuko Wa Dhamana ulio bora nchini Tanzania ambao kwa ufanisi unahamasisha, unasaidia na kuunga mkono miradi na shughulu za jamii katika Nyanja za elimu, afya, kilimo, maji na kupambana na umasikini.

DHAMIRA

Kutafuta raslimali za kutosha kwa ajili ya kusaidia miradi na shughuli za jamii zinazolenga kuinua, kuendeleza na kuunga mkono hali ya maisha ya uchumi endelevu katika jamii ya North Mara kwa muda mrefu mbeleni hata baada kumalizika na kufungwa kwa shughuli za mgodi.
Mengine zaidi kuhusu NMCTF
Mfuko wa dhamana wa North Mara ni matokeo ya mgongano wa kimaslahi baina ya Keng’anya Enterprises Limited (KEL) yenye hati usajili namba 17118 na Placer Dome (T) Limited (PDT) yenye hati ya usajili namba 23446 (awali ilijulikana kama Afrika Mashariki Gold Mines Limited na sasa ni African Barrick Gold). Mgongano huu unarejea shauri nambari 298 ya mwaka 1997 na 315 ya mwaka 2002 yaliyoamuliwa nje ya mahakama na kusajiliwa mahakama kuu ya Tanzania, mnamo mwezi Desemba 2004.

KEL na PDT pamoja na mambo mengine, walikubaliana kuanzisha Mfuko wa Dhamana uliotarajiwa kuanza Januari 2006 kwa ajili ya kusaidia vijiji vitano vya Kerende, Nyangoto, Nyamwaga, Genkuru na Kewanja vilivyo na mkataba na mgodi wa North Mara.
Mfuko ulisajiliwa tarehe 28 Mei 2012 nchini Tanzania chini ya sheria ya nchi namba 318 ihusuyo usajili wa udhamini na kupatiwa hati ya usajili namba 4445 kama hatua ya kutekeleza hukumu ya mahakama kuu ya Tanzania iliyoamua kuanzishwa mfuko ifikapo Januari 2006. Ulianza rasmi mnamo mwezi wa Septemba 2012 ambapo kikao cha kwanza cha Bodi ya Wadhamini kilikutana. Ilipofika mwezi Aprili 2013, mfuko uliajiri watumishi wa kwanza wa Mfuko na kuanza shughuli zake rasmi.
● Lengo kuu la Mfuko wa Dhamana ni kusaidia na kuleta manufaa ya kijamii kwa kutekeleza miradi na shughuli mbalimbali katika jamii inayozunguka mgodi wa North Mara. Miradi na shughuli mabalimbali zinazolengwa hapa ni ya: Afya, Elimu, kilimo, maji, mafunzo, uwezeshaji na kusaidia kuondoa umaskini.
● Kuondoa utofauti na utengano miongoni mwa jamii ya vijiji vitano vinavyozunguka mgodi
● Kuijengea jamii uwezo wa kiuchumi.
● Kuhamasisha makampuni au watu wengine wanaopokea mirahaba na wakandarasi wanaofanya biashara na mgodi wa North Mara kuchangia mfuko.
● Kuchambua na kuamua kwa makini ni wapi pa kuwekeza ili kupata faida
Shughuli kuu ya mfuko ni kuhamasisha, kusaidia na kutoa msukumo kwenye miradi na shughuli katika nyanja za elimu, mafunzo, afya, kujenga uwezo, kilimo, maji na kuondoa umasikini kadiri wadhami watakavyoona yafaa.

Ili kutekeleza majukumu hayo, na pia kuepuka kumaliza fedha za mfuko, ilikubaliwa kwamba, mtaji utokanao na michango utumike katika uendelezaji wa sekta binasi, kupitia uwekezaji kwa kufanya kazi moja kwa moja na sekta binafsi au kupitia taasisi zilizopo kwa nia thabiti ya kupata faida kutokana na riba ya uwekezaji, ili kuufanya mfuko uwe endelevu. Mfuko pia utafikiria kuwekeza kwenye Dhamana za serikali na amana za Benki ili kutekeleza adhma ya uwekezaji.
Wachangiaji pekee katika huu mfuko (wafadhili) hadi sasa ni wawili tu; NORTH MARA GOLD MINES (NMGM) pamoja na KENG’ANYA ENTERPRISES (KEL). Vijiji havijawahi kuchangia huu mfuko na wala hakuna kiasi chochote cha fedha zitokanazo na mrahaba wa vijiji zilizowahi kuingizwa na mgodi katika mfuko huu.

Wanufaikaji wa mfuko huu ni vijiji vitano vinavyozunguka mgodi wa North Mara, ambavyo ni; Nyangoto, Kewanja, Genkuru, Nyamwa-ga na Kerende.
Mfuko unao uongozi ulioundwa kwa mujibu wa kanuni na sharia za nchi kama ilivyoainishwa kwenye sheria ya nchi namba 318 ihusuyo usajili wa udhamini.

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko
Bodi inaundwa na wajumbe sita walioteuliwa kwa kuzingatia kifungu cha 7.1 cha katiba ya mfuko kama ifuatavyo:
2- kutoka Kenganya Enterprises (KEL)
2- kutoka mgodi wa North mara (NMGM)
2- kutoka ndani ja jamii ya vijiji 5

Vikundi Kazi (Working Committees)
Hawa ni wajumbe wawakilishi wa mfuko walioteuliwa na halmashau- ri za vijiji husika. Wajumbe hawa huisadia bodi kutekeleza majukumu yake kwenye maeneo (Vijiji) wanayotoka.

Waajiriwa wa Mfuko
Hawa ni watumishi walioajiriwa na Bodi kwa kuzingatia katiba ya mfuko na sharia zingine za nchi zinazohusika na ajira. Wanafanyakazi kwa kanuni na taratibu zilizowekwa na Bodi na kwa kuzingatia sharia ya ajira na sharia zingine za nchi. Watumishi hawa huwajibika kwenye Bodi ya mfuko.
Tangu kuanza shughuli zake rasmi, mnamo April 2013, Mfuko umeweza kujiendesha kwa mafanikio, ambapo miradi kadhaa imeweza kutekelezwa ndani ya jamii kama ifuatavyo:

1. Ufadhili wa wanafunzi masomo ya Elimu ya juu
Kuanzia Mwaka 2014, Mfuko umefadhili wa wanafunzi katika ngazi za A Level (kidato cha 5&6) - wanafunzi 29 na vyuo vya Elimu ya juu (vyuo vikuu) - wanafunzi 107 kutoka baadhi ya vijiji vya wanufaikaji. Jumla 136 hadi sasa.
Kwa mwaka wa masomo 2017/18, Mfuko umefadhili jumla ya wanafunzi 94, wa A-Level 13 na wa vyuo vikuu 81.

2. Ufadhili wa vikundi vya Kuondokana na umaskini
TIGITE SACCOS iliyopo kijiji cha Nyamwaga kwa ajili ya kuhudumia wakazi wa vijiji vya Nyamwaga na Genkuru na KEMA Group iliyopo kijiji cha Kewanja kwa ajili ya kuhudumia vijiji vya Kata za Matongo na Kemambo.

3. Kuanzisha Maabara za Kompyuta
Mfuko umeweza kuanzisha maabara za kompyuta katika shule za eneo la North Mara. Tumefanikiwa Kuweka Maabara katika shule tisa (9), tano za Msingi na nne za Sekondari.

4. Teknolojia Ya Habari Na Maelezo (TEHAMA)
Tarehe 22/02/2016, Mfuko ulizindua Mradi wa TEHAMA katika shule zinazozunguka Mgodi wa North Mara. Mgeni rasmi katika uzinduzi huu alikuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara Ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof. Simon Msanjila.

5. Mabweni Ya Wasichana
Mfuko umefanikiwa kujenga mabweni ya kisasa kwa ajili ya Wasichana katika Shule za Sekondari za Bwirege na Kemambo. Mabweni haya pia yamejengewa majengo yenye vyoo, mabafu na sehemu za kufuli (Ablution Blocks). Pia yamejengewa matanki ya kuvunia maji ya mvua yenye uwezo wa lita 50,000 kwa kila bweni.

6. Uwekezaji katika Kilimo cha Miwa
NMCTF ni sehemu muhimu katika kilimo cha miwa kinacho tarajiwa kuanza katika wilaya ya Tarime, ikiwa ni sehemu ya uanzishwaji wa kiwanda cha Sukari.
Kuwa na mikakati mahsusi ya uwekezaji ambayo itaufanya Mfuko uboreke kimapato, mwaka hadi mwaka. Wadhamini na uongozi kwa muda wote watakuwa macho kuangaza fursa mpya za uwekezaji ambazo zitaleta mapato mazuri kwa lengo la kuhakikisha kwamba mfuko unaimarika na kuwa endelevu.
● Je ni kweli kwamba asilimia moja ya vijiji imo ndani ya mfuko?
Jibu ni HAPANA. Vijiji havijawahi kuchangia fedha yoyote katika mfuko wala hakuna fedha yoyote ya mrahaba wa vijiji iliyowahi kuingizwa na mgodi katika mfuko.

● Je mfuko unalipia wanafunzi karo za shule?
Kuanzia mwaka 2014, Mfuko uliweka utaratibu maalumu ambao utahakikisha kwamba wanafunzi wanaofaulu vizuri katika mitihani ya kuhitimu kidato cha 4 na cha 6 kwa madaraja ya juu na hasa wanaotoka kwenye familia zenye uwezo duni au mdogo kifedha wanapatiwa ufadhili na mfuko.

● Je, mfuko umechukuwa nafasi ya Mgodi katika miradi ya jamii?
Jibu ni HAPANA. Mgodi utaendelea na majukumu yake ya kutoa huduma kwa jamii kama ilivyo kwenye makubaliano ya mgodi na vijiji vinavyozunguka mgodi.

● Je, Mfuko unatoa mikopo kwa mtu mmoja mmoja au vikundi?
Jibu ni HAPANA. Mfuko hautoi mikopo kama habari ilivyoenea mitaani. Mfuko haujakaa katika muundo wa taasisi za kifedha na hivyo hautoi mikopo kwa sasa.
Hata hivyo, Mfuko unatambua changamoto ya hali ngumu ya kiuchumi inayoikabili jamii yetu ya North Mara, na tunajaribu kila liwezekanalo kuona ni jinsi gani ya kusaidiana na jamii katika kuikabili changamoto hii.